Kamati ya Fedha na Utawala Halmashauri ya Mji wa Mbulu imekagua miradi yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1.5, Fedha zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2024/25

Fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa, Mabweni na vyoo katika shule tatu za Sekondari.

Katika ukaguzi wa miradi hiyo, Kamati imeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mhe. Peter Sulle na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay, na Waheshimiwa Madiwani ambao ni wajumbe wa kamati hiyo wameagiza kuharakishwa kwa ujenzi wa miradi hiyo hususani Madarasa, mabweni na vyoo katika shule ya Sekondari Marrang, Tlawi, Imboru na shule ya Msingi Laghandamur.
Aidha Viongozi hao wameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi za miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu.

Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.