• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe kwa wafanyakazi |
Halmashauri ya Mji Mbulu
Halmashauri ya Mji Mbulu

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Biashara Viwanda na Uwekezaji
      • Mipango na Uratibu
      • Kilimo Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • UKAGUZI WA NDANI
      • USIMAMIZI WA MANUNUZI
      • FEDHA NA UHASIBU
      • MAWASILIANO SERIKALINI
      • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
      • HUDUMA ZA SHERIA
      • UHIFADHI WA MALIASILI NA MAZINGIRA
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
  • Machapisho
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Kituo cha Habari
    • Press Release
    • Video
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Matukio
  • Miradi
    • Approved Project
    • Ongoing Project
    • Completed Project
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma kwa watumishi
    • Maij
    • Elimu
    • Uvuvi
  • Kata
    • Ayamaami
    • Ayamohe
    • Bargish
    • Daudi
    • Endagikot
    • Gehandu
    • Gunyoda
    • Imboru
    • Kainam
    • Marangw
    • Murray
    • Nahasey
    • Nambis
    • Sanubaray
    • Silaloda
    • Tlawi
    • Uhuru
  • Uwekezaji
  • Madiwani

MADIWANI WAMETAKIWA KUJIKITA KATIKA UTATUZI WA KERO ZA WANANCHI KATIKA KATA.

Posted on: February 12th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga, amewataka Madiwani wa Wilaya ya Mbulu kuwa mstari wa mbele katika kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo yao, akisisitiza kuwa uongozi wao upimwe kwa uwezo wa kuleta suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi.


Ameyasema hayo leo, Februari 12, 2026, wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Madiwani yaliyofanyika kuanzia Februari 11 hadi 12, 2026, yakijumuisha Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.


Akizungumza katika mafunzo hayo, Mhe. Sendiga alieleza kuwa Madiwani ni kiungo muhimu kati ya Serikali na wananchi, hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Halmashauri pamoja na misingi ya utawala bora.


Aliwahimiza kufanya mikutano ya mara kwa mara na wananchi kwa kuzingatia vipaumbele vya maendeleo, ili kusikiliza changamoto zao na kupanga mipango ya utekelezaji kwa pamoja.


“Rudini kwa wananchi wenu, sikilizeni kero zao na zipatieni ufumbuzi. Msikubali kuwa sehemu ya malalamiko; kuweni sehemu ya suluhisho,” alisisitiza Mhe. Sendiga.


Aidha, aliwataka Madiwani kujiwekea malengo mahsusi katika utekelezaji wa shughuli za Serikali na kuhakikisha wanakuwa wasimamizi madhubuti wa maendeleo katika kata zao.


Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Aliwataka Madiwani kuwa wabunifu katika kubuni na kupanua vyanzo vipya vya mapato, pamoja na kusimamia rasilimali zilizopo kwa ufanisi, uwazi na uadilifu.


Mhe. Sendiga alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kusisitiza uwajibikaji, usimamizi thabiti wa rasilimali za umma na utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Hivyo, aliwataka Madiwani kwenda kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uzalendo na kujituma ili kuendana na dhamira ya Serikali ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.


Mafunzo hayo yamelenga kuwaimarisha Madiwani katika misingi ya uongozi na utawala bora ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya uwakilishi na usimamizi wa maendeleo ya wananchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 July 04, 2025
  • TANGAZO MUHIMU KUTOKA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHUSU MAOMBI YA MPIGA KURA. September 15, 2025
  • TANGAZO LA HUDUMA ZA KIBINGWA KUANZA KUTOLEWA MBULU MJI May 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MJI WA MBULU June 09, 2025
  • Ona zote

Habari mpya

  • MADIWANI WAMETAKIWA KUJIKITA KATIKA UTATUZI WA KERO ZA WANANCHI KATIKA KATA.

    February 12, 2026
  • MAFUNZO ELEKEZI YA MADIWANI WA WILAYA YA MBULU

    February 11, 2026
  • ELIMU YA BIMA YA AFYA KWA WOTE YATOLEWA KWA WANANCHI

    February 10, 2026
  • TUPANDE MITI ILI KUTUNZA NA KUHIFADHI MAZINGIRA YETU- Mhe. Lohi

    February 11, 2026
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN BUNGENI
More Videos

Tovuti mashuhuri

  • Babati dc Website
  • Hanang' dc Website
  • Babati Town Website
  • Simanjiro Website
  • Kiteto Website
  • Mbuludc Website

Tovuti Mbadala

  • Tamisemi
  • Ikulu
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • Mbulu Tc Facebook
  • Mbulu Town Council WatsApp
  • Mbulu Tc Instagram

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.