• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe kwa wafanyakazi |
Halmashauri ya Mji Mbulu
Halmashauri ya Mji Mbulu

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Biashara Viwanda na Uwekezaji
      • Mipango na Uratibu
      • Kilimo Mifugo na Uvuvi
      • Elimu ya Awali na Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Miundombinu na Maendeleo ya Vijiji na Miji
      • Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • UKAGUZI WA NDANI
      • USIMAMIZI WA MANUNUZI
      • FEDHA NA UHASIBU
      • MAWASILIANO SERIKALINI
      • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
      • HUDUMA ZA SHERIA
      • UHIFADHI WA MALIASILI NA MAZINGIRA
      • USIMAMIZI WA TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
  • Machapisho
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Acts
    • Application Forms
  • Kituo cha Habari
    • Press Release
    • Video
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Matukio
  • Miradi
    • Approved Project
    • Ongoing Project
    • Completed Project
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma kwa watumishi
    • Maij
    • Elimu
    • Uvuvi
  • Kata
    • Ayamaami
    • Ayamohe
    • Bargish
    • Daudi
    • Endagikot
    • Gehandu
    • Gunyoda
    • Imboru
    • Kainam
    • Marangw
    • Murray
    • Nahasey
    • Nambis
    • Sanubaray
    • Silaloda
    • Tlawi
    • Uhuru
  • Uwekezaji
  • Madiwani

TUPANDE MITI ILI KUTUNZA NA KUHIFADHI MAZINGIRA YETU- Mhe. Lohi

Posted on: February 11th, 2026


Diwani wa Kata ya Sanubaray, Mhe. Emmanuel Lohi, ametoa wito kwa wananchi, walimu na wanafunzi kushiriki kikamilifu katika upandaji na utunzaji wa miti kama hatua muhimu ya kulinda mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.


Mhe. Lohi ameyasema hayo leo Februari 10, 2026, wakati wa zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Shule ya Msingi Guwangw, ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya upandaji miti katika taasisi za Serikali, pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali katika uhifadhi wa mazingira na rasilimali za asili.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Lohi alisisitiza kuwa upandaji miti si tukio la siku moja, bali ni mchakato endelevu unaohitaji usimamizi, ufuatiliaji na utunzaji wa karibu ili miti hiyo iweze kukua na kuleta manufaa yaliyokusudiwa.



“Tunapanda miti ili kutunza mazingira yetu yanayotuzunguka. Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha miti hii inatunzwa vizuri, kwani itatusaidia kuboresha hali ya hewa, kuzuia mmomonyoko wa udongo na kuimarisha afya ya jamii yetu,” alisema Mhe. Lohi.


Aidha, aliwahimiza walimu kuendelea kuwajengea wanafunzi utamaduni wa kupenda na kutunza mazingira tangu wakiwa wadogo, akieleza kuwa elimu ya mazingira ni msingi muhimu wa maendeleo endelevu ya Taifa.



Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Guwangw,Mwl. Saymon Kissimbi,ameahidi kusimamia ipasavyo utunzaji wa miti hiyo kwa kushirikiana na walimu na wanafunzi, ili kuhakikisha inakua na kuleta tija katika mazingira ya shule. Ameeleza kuwa zoezi hilo limekuwa funzo muhimu kwa wanafunzi kuhusu uwajibikaji na umuhimu wa kulinda mazingira.



Jumla ya miti 70 imepandwa katika Shule ya Msingi Guwangw, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa juhudi za kuhifadhi mazingira na kuimarisha uoto wa asili katika Kata ya Sanubaray.



Zoezi hilo linaendelea katika taasisi mbalimbali za Serikali na linatarajiwa kuongeza mwamko wa jamii kuhusu umuhimu wa upandaji na utunzaji wa miti kwa maendeleo endelevu.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 July 04, 2025
  • TANGAZO MUHIMU KUTOKA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHUSU MAOMBI YA MPIGA KURA. September 15, 2025
  • TANGAZO LA HUDUMA ZA KIBINGWA KUANZA KUTOLEWA MBULU MJI May 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MJI WA MBULU June 09, 2025
  • Ona zote

Habari mpya

  • MAFUNZO ELEKEZI YA MADIWANI WA WILAYA YA MBULU

    February 11, 2026
  • ELIMU YA BIMA YA AFYA KWA WOTE YATOLEWA KWA WANANCHI

    February 10, 2026
  • TUPANDE MITI ILI KUTUNZA NA KUHIFADHI MAZINGIRA YETU- Mhe. Lohi

    February 11, 2026
  • MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI ROBO YA PILI 2025/2026

    January 30, 2026
  • Ona zote

Video

HOTUBA YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN BUNGENI
More Videos

Tovuti mashuhuri

  • Babati dc Website
  • Hanang' dc Website
  • Babati Town Website
  • Simanjiro Website
  • Kiteto Website
  • Mbuludc Website

Tovuti Mbadala

  • Tamisemi
  • Ikulu
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • Mbulu Tc Facebook
  • Mbulu Town Council WatsApp
  • Mbulu Tc Instagram

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.