Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu Leo 16/06/2025 alipozungumza na Wananchi wa Kata ya Ayamaami ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
" Wazazi na jamii nzima tunalo jukumu la kushiriki kikamilifu katika suala zima la malezi na makuzi ya watoto kwa kuzingatia haki na Usawa". Alisema Mhe. Michael Semindu
Sambamba na hayo Mhe. Semindu amesisitiza kuendelea kuwalea watoto kwa kuzingatia maadili ya kiafrika ili kujenga kizazi bora kijacho.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi.Rehema Bwasi ameeleza kuwa katika jitihada za kupambana na ukatili wa kijinsia Halmashauri imeendelea kuunda madawati kwa ngazi za kata.
"Jamii imeendelea kupewa elimu juu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto kupitia makongamano mbalimbali". Alisema Bi. Rehema
Kwa upande wake kiongozi wa Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo Mchungaji Augustino Halule ameeleza kuwa elimu juu ya ukatili imeendelea kutolewa kwa Waumini ili kupunguza kasi ya ukatili katika Wilaya ya Mbulu.
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yamekuwa na Kaulimbiu isemayo “Haki za mtoto; Tulipotoka, Tulipo na Tuendako.”
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.