Wazazi na walezi wametakiwa kuhakikisha watoto wenye wiki 14 na wenye umri wa miezi 9 wanawapeleka watoto wao vituo vya kutolea huduma za Afya ili waweze kupata Chanjo ya Polio.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bw. Paulo Bura akiwa mgeni rasmi kwenye Kikao kilichofanyila leo 24 Aprili, 2025 ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kujadili ongezeko la Chanjo ya polio kwa watoto.
“Chanjo hii haihusiani kabisa na masuala ya imani za kishirikina, hivyo niwasihi wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ili wapate Chanjo hii muhimu kwa ajili ya kulinda Afya zao”. Alisema Ndugu. Bura
Wakati huo huo amesisitiza Elimu kuendelea kutolewa kwa Wananchi kuhusu magonjwa na Chanjo mbalimbali ikiwemo ya Polio ili wananchi waweze kujitokeza kwa wingi kupata huduma za Afya zinazotolewa na Serikali.
Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Ndugu. John Faustin amesema zoezi hili litafanyika kuanzia tarehe01 Mei 2025 huku akiendelea kuwahimiza Wazazi na walezi kushiriki kikamilifu ili kufanikisha zoezi hili muhimu kwa Afya za Watoto.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Wahudumu wa Afya ya Msingi, Viongozi wa dini,Wataalamu wa Halmashauri na Wazee maarufu.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.