Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu leo Juni 11, 2025 wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa Utendaji kazi kwa Watumishi wa Umma( e-utendaji) katika ukumbi wa Halmashauri ya mji wa Mbulu.
Akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu amewaeleza watumishi hao kuwa wasikivu kwani ndiyo mfumo unaotoa tathmini ya utekelezaji wa Majukumu ya Kila siku.
“Mfumo huu utatutejenga na kutatua changamoto ambazo tumekuwa tukikutana nazo kila mara lakini pia kila mmoja ataweza kutambua dosari ambazo amekuwa akizifanya”. alisema Bi. Rehema
Kwa upande wake Mkufunzi kutoka OR MUUUB ameeleza kuwa ni muhimu kuzingatia ujazaji wa utekelezaji wa majukumu ikiwemo kuandaa mpango kazi na ufuatiliaji wa mapango kazi mpaka tamati.
Bi. Elizabeth ameongeza kwa kuwaeleza watumishi kuwa mfumo huo unatumiwa katika upandishaji wa madaraja kwa watumishi.
“Ni haki ya kila mtumishi kupanda daraja kwa wakati uliokusudiwa hivyo watumishi wote ni muhimu kushiriki katika kujaza taarifa za utekelezaji wa Majukumu.”Alisema Bi. Elizabeth
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Wakuu wa Idara na vitengo pamoja na wakuu wa Sehemu wakiwemo wakuu wa shule za msingi na Sekondari na Waganga wafawidhi wa Zahanati na vituo vya afya.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.