
Mei 29, 2025 Watumishi wa Ajira mpya Halmashauri ya Mji wa mbulu wamepatiwa Mafunzo ya Mfuko wa hifadhi ya jamii (PSSSF).
Akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo hayo Kaimu Mkuu wa Idara ya Utumishi na Usimamizi wa Rasilimali watu Halmashauri ya Mji wa Mbulu Kulthum Seif
ameeleza umuhimu wa mafunzo ya PSSSF kwa watumishi na amewasisitiza kuwa makini kwenye mafunzo yatakayo tolewa.
“Taasisi imeona ni muhimu mkapewa mafunzo haya ili yaweze kuwasaidia katika Utumishi wa Umma”. Alisema Bi. Kulthum
Sambamba na hayo Bi. Kulthum amewasisitiza watumishi wote kuendelea kutii sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma.
Kwa upande wake Meneja wa PSSSF Mkoa wa Manyara Ndugu. Harson Werema Ndugu amesema kujiunga na Mfuko wa Huduma za jamii kwa Watumishi kutawasaidia kupata mafao baada ya kustaafu lakini pia huduma kadha wakadha katika kipindi cha utumishi.


Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.