Mratibu wa Elimu Kata ya Uhuru Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mwl. Athanasia Ngowi akiwa ameambatana na Watendaji wa Mitaa amekagua mahudhurio ya wanafunzi kuripoti shuleni baada ya shule zote kufunguliwa leo Julai 8 nchi nzima.
Kwa nyakati tofauti Mratibu Mwl. Athanasia amewataka wanafunzi wote kuacha tabia ya utoro na kuhudhuria shuleni sambamba na kuingia darasani tayari kwa kuanza masomo ambayo yameanza rasmi leo Julai08,2025.
Mbali na utoro amewasisitiza walimu kuanza kufundisha bila kukosa kipindi chochote ili waweze kwenda na ratiba iliyowekwa jambo litakalosaidia kumaliza silabasi kwa wakati.
Wakiwa katika shule ya Msingi Waama Mtendaji wa Mtaa wa Buwa Bi. Mariam Mtani na Mtendaji wa Mtaa Maringo Bi. Angela Kanile wamewakumbusha na kuwasisitiza wazazi kuona umuhimu wa upatikanaji wa chakula shuleni katika kipindi chote cha muhula wa masomo na wakikemea suala la utoro kwa wanafunzi wote.
"Chakula ni muhimu shuleni kawakumbusheni wazazi kutimiza ahadi ya kuleta chakula kama tulivyokubaliana " walisema.
Shule zilizotembele wa ni shule ya Msingi Harka na Shule ya Msingi Waama.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.