Timu ya Wataalamu wa Afya wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Dr. Martin Lohay wametembelea Kituo cha Afya Daudi na Tlawi kwa ajili ufuatiliaji wa utoaji huduma kwa watoto waliozaliwa kabla ya Muda (Watoto njiti).
Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto Bi. Swaumu Cosmas amewasisitiza watoa huduma kwenye vituo vya Afya kuzingatia taratibu zote katika utoaji wa huduma kwa wazazi na watoto waliozaliwa kabla ya wakati ili kulinda afya ya mama na mtoto.
“Tukiwa wahudumu wa afya tuna jukumu la kumlinda mama na mtoto kwani ni kipindi ambacho wanahitaji uangalizi wa karibu kutoka kwetu”. Alisema Bi. Swaumu
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Dr. Martin Lohay amewasisitiza wataalamu kuwasilisha changamoto wanazokumbana nazo katika utoaji wa huduma kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda ili ziweze kutatuliwa kwa haraka.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.