WANUFAIKA WA MIKOPO 10⁒ MBULU MJINI WASISITIZWA KUTUMIA MIKOPO KWA MALENGO YALIYOKUSUDIWA.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael John Semindu Oktoba 8,2025 akikabidhi Pikipiki 05 na vyeti kwa vikundi 18 vinavyojumuisha Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu yenye thamani ya shilingi milioni Sitini na Sita na laki tano (66,500,000/=)katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Mhe. Semindu amewasisitiza wanufaika wa mikopo hiyo kuutumia mikopo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuzaliwa kulingana na shughuli wanazozitekeleza ili kuwanufaisha na kuzirejesha kwa wakati ili kuwanufaisha makundi mengine.
“Serikali imelenga kuinua uchumi wa kila mmoja ndiyo maana inatenga fedha kwaajili ya mikopo isiyokuwa na riba kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu”. alisema Mhe. Semindu
Kwa upande wao, baadhi ya wanufaika wameishukuru serikali kwa kuendelea kuwaamini vijana, wanawake na watu wenye ulemavu wakiahidi kutumia mikopo hiyo kama nyenzo ya kujenga biashara na ajira endelevu.
Hundi, pikipiki na vyeti vimekabidhiwa katika hafla ya iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.