


WANANCHI TUMIENI FURSA YA CLINIKI YA MADAKTARI BINGWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIAFYA-RC SENDIGA
Mkuu wa Mkoa Wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amewasihi Wananchi wa Wilaya ya Mbulu na Mikoa jirani Kutumia fursa ya Cliniki ya madaktari Bingwa wa ndani ya Mkoa wa Manyara.
Ameyasema hayo Desemba 16,2025 wakati wa uzinduzi wa kambi ya madaktari Bingwa wa ndani ya mkoa wa Manyara iliyofanyika katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
“Lengo la kuwa na kliniki ya madaktari bingwa ndani ya mkoa ni kupunguza gharama kwa wananchi kufata huduma za matibabu nje ya mkoa”,alisema Mhe. Sendiga
Mhe. Sendiga aliongeza kusema, Mkoa wa Manyara unajivunia mafanikio makubwa ya serikali pamoja na maendeleo ya teknolojia juu ya uwepo wa vifaa tiba vya kisasa ameeleza kuwa huduma zimeendelea kuimarika kila siku.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu alitoa shukrani kwa serikali ya awamu ya sita na uongozi wa mkoa wa Manyara kwa kuendelea kuboresha huduma za afya na kusogeza huduma karibu na Wananchi wa Wilaya ya Mbulu.
Kwa niaba ya Wananchi wengine Bw. Nadee alitoa shukrani kwa Serikali na uongozi wa mkoa kwa kliniki maalumu ya madaktari Bingwa huku akiwasisitiza Wananchi wengine kujitokeza kupata huduma kwa karibu na kwa bei nafuu.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.