Kamati ya Fedha na Utawala wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu imewapongeza Wananchi Wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwa kuendelea kushiriki katika Miradi ya Maendeleo.
Akizungumza katika Ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala Mhe. Peter Sulle ameeleza Kuwa kushiriki katika Shughuli za Maendeleo ni kuunga Mkono Jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoa fedha nyingi kwa lengo la Kusogeza Huduma karibu na Wananchi hivyo tuendelee kushirikiana”.Alisema Mhe. Sulle
Sambamba na hayo Mhe. Sulle amewapongeza Walimu kwa kuendelea kusimamia Miradi ya Maendeleo pamoja na Kusimamia nidhamu ya Wanafunzi kwa ujumla.
Kwa niaba ya Wananchi Ndugu.Barnabas Yamay ametoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwaajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Nae Kaimu Mkurugenzi Ndugu. Zabron Marwa ameahidi kuendelea kushirikiana ili kusongeza gurudumu la maendeleo ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Kamati ya fedha imefanya ziara katika Shule mpya ya Sekondari Hylot(Tloma),Shule mama Ya Hyloto,Ujenzi wa vyumba vinne vya Madarasa Shule ya Msingi Kuta na Ujenzi wa Bwalo,Mabweni mawili,matundu kumi ya Vyoo na Vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Kainam.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.