Wananchi, wafanyabiashara na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu wamefanya usafi wa mazingira ambao hufanyika kila juma la mwisho wa mwezi.
Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 22 Februali, 2025 katika maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu ambapo wananchi wameshiriki zoezi hilo katika maeneo ya makazi yao huku wafanyabiashara wakishiriki zoezi hilo kwenye maeneo yao ya biashara.
Wakati huohuo, watumishi waliopo Makao makuu ya Halmashauri wakishiriki zoezi hilo katika majengo ya Halmashauri na Dampo la Taka wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Rehema Bwasi.




Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.