Katika mwendelezo wa juhudi za kuwafikia wananchi kupitia elimu ya jamii, leo juni 09,2025 Kata ya Imboru imepata fursa ya kupata elimu kutoka katik kitengo cha Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Imboru Ndugu. Tomic Simbeye ameeleza kuwa Mafunzo hayo yamekuwa chachu ya mabadiliko chanya kwa jamii.
“Elimu zote zinazotolewa kwa jamii zinalenga kupinga ukatili wa kijinsia, kupunguza au kutokomeza kabisa mimba za utotoni, kuhakikisha jamii nzima inaishi katika haki na usawa n.k.” Alisema Ndugu. Simbeye
Sambamba na hayo Ndugu. Simbeye alieleza kuwa kuelekea siku ya mtoto wa Afrika wazazi na walezi wanalo jukumu la kuhakikisha watoto wanalelewa katika malezi bora kwa kuzingatia haki na usawa.
Kwa upande wake Mratibu wa Dawati la msaada wa kisheria wa Mama samia(Mama Samia legal aid compaign) Ndugu. Angel Wilson amewasisitiza Wananchi wote kuendelea kushirikiana ili kutatua migogoro iliyopo katika jamii ili kutimiza adhma ya serikali ya kuhakikisha Wananchi wote wanadumisha amani, upendo na utulivu.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.