


Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Ndugu. Crispin Chalamila katika Hafla ya Uzinduzi wa Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Mbulu iliyofanyika Novemba 25, 2025.
Akizungumza na Wananchi na Wadau mbalimbali wa Wilaya ya Mbulu Ndugu.Chalamila amewasisitiza Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na Wataalamu wa TAKUKURU katika utoajia wa taarifa za Rushwa.
“Ushirikiano katika Utoaji wa vitendo vya rushwa utaongeza Uwazi na Uwajibikaji Pamoja ka kuzuia mianya ya Rushwa katika jamii yetu , hivyo Wanachi tunatakiwa kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya rushwa”,alisema Ndugu. Chalamila
“Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa itaendelea kutoa elimu ya madhara ya Rushwa kwa Wananchi kupitia majukwaa mbalimbali pamoja na sanaa,lengo ni kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na uelewa wa pamaoja kuhusu Rushwa.
Naye, Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Manyara Ndugu. Bahati Haule amewaeleza Wananchi kuwa TAKUKURU itaendelea kuwa karibu na Wananchi ili kuhakikisha Miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na kutoa huduma kwa Wanachi kama ilivyopangwa na Serikali na ameeleza uwepo wa Ofisi katika Wilaya ya Mbulu utaongeza wadau wa wa kuzuia na kupambana na Rushwa.
Kwa Upande Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu amaeahidi kuendelea kushirikiana na TAKUKURU ili kukomeza vitendo na mianya yote ya Rushwa katika Wilaya ya Mbulu na kuhakikisha Wananchi wanahudumiwa kwa kwa haki na Usawa.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.