Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay amefanya hafla fupi ya kukabidhi gari la kubeba wagonjwa kwa wananchi wa Tarafa ya Daudi yenye jumla ya Kata 3 (Daudi, Marangw na Bargish)
Akizungumza na Wananchi wa Tarafa hiyo Mhe. Isaay ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Wananchi gari jipya la kubebea wagonjwa (Ambulance)
“Niwaambie wananchi wenzangu wa Tarafa hii ya Daudi sisi tumependelewa sana kwani kwa upande wa afya kila sekta imeboreshwa kwa hiyo hatuna budi kutoa
shukrani zetu za Dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upekee wake katika kusaidia sekta hii muhimu ya Afya kwenye Tarafa yetu”.Alisema Mhe.Isaay
Aidha, Mhe.Isaay ameongeza kwa Kuwasisitiza wananchi kwenda kuwa mabalozi kuyasema yale mazuri yote yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya Sita.
Kwa niaba ya Wananchi wengine, Cresent Bura mkazi wa Daudi ametoa shukurani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya sita na kuongeza kuwa gari la wagonjwa litapunguza kadhia iliyokuwa ikiwakumba hasa kwa kina mama wajawazito.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Ndugu. Gideon Kitoboli ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuboresha huduma za Afya na ametoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Mbulu mjini kwa kuendelea kuwasemea Wananchi wa Jimbo la hilo linalokua kwa kasi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Hafla hiyo ya kukabidhi gari la Wagonjwa kwa Tarafa ya Daudi imefanyika katika Kituo cha Afya Daudi kata ya Daudi kijiji cha Moringa.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.