



Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Michael Semindu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bweni la Wavulana katika Shule ya Sekondari Kainam, Desemba 01, 2025.
Mhe. Semindu amewasisitiza wanafunzi kuendelea kutunza miundombinu hiyo ili iweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu.
“Serikali inaleta fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wote mnakuwa katika mazingira salama na rafiki, hivyo tunzeni miundombinu yote,” alisema Mhe. Semindu.
Aidha, Mhe. Semindu amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuwa na nidhamu wawapo shuleni na nyumbani, akibainisha kuwa mafanikio ya elimu yanaenda sambamba na nidhamu binafsi.
Kwa niaba ya wanafunzi wote, Kaka Mkuu wa Shule hiyo, Samwel Stephano, ametoa shukrani kwa Serikali kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia, akisema kuwa hatua hiyo ni chachu ya mafanikio katika elimu.
Kwa upande wake, Mkuu wa shule hiyo, Mwl. Emmanuel Madme, ameushukuru uongozi wa Halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ushirikiano waliouendelea nao katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi wa bweni la wavulana pamoja na miradi mingine ya shule hiyo.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.