Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi. Rehema Bwasi leo Mei 13,2025 amepokea ugeni kutoka Wizara ya Elimu na Taasisi ya Elimu ya watu wazima, Wafadhili kutoka Jamhuri ya watu wa Korea na Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Manyara waliotembelea Mbulu kwa lengo la kuona Maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya Ufundi kwa Vijana.
Karakana hiyo ya ufundi stadi inajengwa kwa ufadhili wa Mradi wa IPOSA ambapo mradi huo unajengwa katika Kituo cha Shule ya Msingi Endagkot.


Lengo la ujio wa Ugeni huu ni kuona maendeleo ya ujenzi wa Karakana ya ufundi kwa Vijana walio na umri wa miaka 14-21 walio nje ya mfumo rasmi wa shule au ambao hawakupata fursa ya Masomo.
Bi. Rehema ameendelea kuishukuru Serikali ya Awamu ya sita kwa kuendelea kuimarisha miundombinu ya elimu.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.