IONGOZI WA NGAZI ZOTE MBULU TC WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA UTOAJI TAARIFA ZA VITENDO VYA KIKATILI.
Rai hiyo imetolewa leo tarehe 30/06/2025 na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe.Michael Semindu alipozungumza na Viongozi wa ngazi zote za Halmashauri ya Mji wa Mbulu katika Kikao cha Kuweka mipango na mikakati ya kukabiliana na vitendo vya kikatili.
"Viongozi wa Serikali tuna wajibu wa kukabiliana na vitendo vyote vya kikatili katika jamii tunazoishi,hivyo mawasiliano ni nyenzo muhimu".Alisema Mhe. Semindu
Sambamba na hayo Mhe.Semindu amewasisitiza viongozi wote kutokupuuza matukio yanayojitokeza katika jamii ikiweo mila na desturi potofu hasa Ukeketaji wa Wanawake.
Kwa Upande wake Kiongozi wa umoja wa makanisa ya kikristo Mchungaji Augustino Halule ameahidi kuendelea kutoa elimu kwa waumini juu ya athari ya vitendo vya vya kikatili katika jamii ili kutokomeza kabisa matukio yote ya kikatili katika Wilaya ya Mbulu.
Kwa Upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia Wilaya ya Mbulu.Glory Nassoni Daud 

amewasisitiza viongozi kuacha tabia ya Kumaliza vitendo vya kikatili kwa ngazi ya jamii pekee bila wahalifu kuchukuliwa hatua.
“Kumekuwa na tabia ya Viongozi wa ngazi ya jamii kupokea rushwa kwa wahalifu wa vitendo vya kikatili kwa lengo la kuahirisha kesi hizo ni unyanyasaji mkubwa ambao watoto wamekuwa wakifanyiwa ni jukumu letu Alisema. Mkuu wa Dawati la Kijinsia Glory Nassoni Daudi.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.