
Kuelekea Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, leo Juni 6,2025 Halmashauri ya Mji wa Mbulu imefanya Kongamano maalumu lililojumuisha zaidi ya Vijana 300 lenye lengo la kuwapa mafunzo ikiwemo kueleza Stadi mbalimbali za Maisha.
Akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Vijana Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu amewataka vijana hao kujitambua na kushirikiana katika masuala yote ya maendeleo ili kuinuana kiuchumi.
“Naomba nitumie wasaa huu kuwakumbusha vijana kuwa Safari ya Mafanikio ni Mchakato hivyo ni jukumu letu sote kuendelea kuelimishana juu ya maisha yetu ya kila siku”.Alisema Mhe.Semindu
Sambamba na Hayo ameongeza kwa kuwasisitiza vijana kushiriki Mbio za Mwenge wa uhuru 2025 na kuelewa jumbe mbalimbali zilizobebwa na Mwenge wa uhuru 2025.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi. Rehema Bwasi amewasisitiza vijana kuzingatia mafunzo yatakayo tolewa na Kwenda kuwa balozi kwa vijana mbalimbali ili kuweza kusaidiana katika maisha ya kila siku.
Kongamano hilo limehusisha vijana kutoka chuo cha uuguzi Mbulu, chuo cha maendeleo ya Wananchi Tango, Shule na sekondari Genda na Gehandu
Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 inasema “Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa Mwaka 2025,kwa amani na utulivu”

Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.