Wataalamu wa Mazingira Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara wametakiwa kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi juu ya utunzaji wa uoto wa asili.
Rai hiyo imetolewa mapema hii leo tarehe 20 Machi, 2025 na wajumbe wa Kamati ya Mazingira na Mipango Miji ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Emmanuel Burra wakiwa katika ziara walipotembelea moja ya kivutio cha utalii cha Mlima Guwangw unaopatikana Kata ya Ayamohe Mtaa wa Guwangw.
Akizungumza na Wajumbe wa Ziara hiyo Mhe. Burra amesisitiza wananchi wote wanaofanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo kuondolewa mara moja kwa ajili ya kutunza uasilia wa Mlima huo.
“Eneo hili linatakiwa kulindwa kwani utunzaji wa uoto huu katika Mlima utasaidia kizazi cha baadaye hivyo ni muhimu kila mmoja kuwa balozi ili kuhakikisha usalama unakuwepo katika eneo hili la mlima”. Alisema Mhe. Burra
Sambamba na hayo Kaimu Mkurugenzi Ndugu. Gidioni Kitoboli ameahidi kuendelea kushirikiana na Kamati ili kufanikisha zoezi la kutoa elimu kwa Wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa uoto wa Asili.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.