Kuelekea Maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa Tanzania, Halmashauri ya Mji wa Mbulu imefanya Bonanza maalumu la michezo leo tarehe 8 Disemba, 2024 katika uwanja wa Halmashauri ya mji wa Mbulu.
Akizungumza na Wananchi wa Mbulu Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mhe.Veronica Kessy amewataka Wananchi kushiriki katika Shughuli muhimu kuelekea maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru.
“Ni muhimu kushiriki katika matukio ya kihistoria kwani yanatukumbusha mahali tulipo,Tulikotoka na tuendako lakini pia tunajua maendeleo katika wilaya yetu”.Alisema Mhe.Kessy
Aidha, amewaeleza wananchi kuwa maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru ni muhimu katika kuenzi juhudi zilizofanywa na waasisi wetu.
Sambamba na hayo Mhe.Kessy amewakumbusha wananchi kujitokeza siku ya Jumatatu tarehe 09 Disemba,2024 katika Mdahalo utakaelezab mambo mbalimbali ya kihistoria na maendeleo ya Taifa.
Bonanza hilo limehusisha michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kamba,kukimbiza kuku,Mchezo wa mpira wa miguu n.k
Maadhimisho ya miaka 63 yana kaulimbiu isemayo “Uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa maendeleo yetu”
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.