Kamati ya UKIMWI( CMAC) Halmashauri ya Mji wa Mbulu imepata mafunzo yanayohusu Ukimwi na mbinu mbalimbali za kutokomeza maambukizi mapya huku ikihamasishwa kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi.
Mafunzo hayo yametolewa kwa wajumbe wa kamati hiyo inayojumuisha viongozi wa Taasisi binafsi, Kidini na Waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mhe. Peter Sulle.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo Mratibu wa UKIMWI Halmashauri ya Mji wa Mbulu Ndugu.Esther Isaya amesema ni muhimu wajumbe hao pamoja kushirikiana kuwaelimisha wananchi kupitia mikutano ya hadhara, Mikusanyiko ya kidini na hata mashuleni ili kupunguza maambukizi mapya yatokanayo na Virusi vya Ukwimwi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mhe. Peter Sulle amesema jukumu la wanakamati ni kuhakikisha wanashirikiana na wataalamu wa ngazi za Vijiji, Kata na Halmashauri kuwafikia wananchi kwenye maeneo yao ili kupambana na UKIMWI
“Kama viongozi wa Taasisi mbalimbali,Taasisi za Dini na Madiwani tunao wajibu wa kutoa elimu kwa wananchi wetu iwe ni Misikiti, Kanisani, Vilabuni, Uwanjani hata Mashuleni juu ya namna nzuri ya kujikinga na maambukizi”.
Vilevile ameendelea kuiasa jamii kutowatenga waathirika kwani kufanya hivyo ni unyanyapaa usio na msingi wowote kwa waathirika jambo ambalo si jema.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.