Timu ya Wataalamu ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu( CMT) imetembelea kuona maendeleo ya Miradi inayotekelezwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu na kushauri kuongezwa umakini katika usimamizi wa fedha za Serikali.
Timu hiyo imesema ili kuwa na miradi yenye ubora ni lazima thamani ya fedha ionekane, hivyo usimamizi wake unapaswa kuwa kwa ukaribu na umakini zaidi hasa katika ununuzi wa vifaa.
Kaimu Mkurugenzi Ndugu. Gidion kitoboli amesisitiza kasi iongezeke kwenye miradi yote inayotekelezwa ili ianze kutumika na Wananchi waendelee kupata huduma inayostahili kama ambavyo Serikali
Ndugu. Kitoboli amesisitiza Mkandarasi anayejenga baadhi ya majengo ya Hospitali hiyo kuhakikisha anatekeleza miradi kwa kufuata miongozo iliyopo kwenye ramani (BOQ)inayoonesha mahitaji ya majengo hayo.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.