Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi. Rehema Bwasi amefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Akiwa katika Ziara hiyo amewasisitiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa Miradi ili ianze kutumika kama ilivyopangwa.
“Dhamira ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha miradi hii inakamilika na ianze kutumika haraka zaidi ni hii miradi ya Elimu ambayo tunapokea wanafunzi wetu siku siyo nyingi tujitahidi kuongeza kasi” Amesema Bi.Rehema.
Miradi iliyotembelewa ni Mradi wa madarasa matatu shule ya Msingi Imboru, Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Imboru, Ujenzi wa madarasa na mabweni shule ya Sekondari Chief Sarrwat.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.