Serikali imesema itaendelea kuimarisha Kamati za MTAKUWA katika ngazi ya Halmashauri, Vijiji na Mitaa Halmashauri ya Mji wa Mbulu ili kufanikisha zoezi la kupambana na ukatili wa Kijinsia
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mhe. Alex Tango ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia yaliyofanyika Kata ya Murray Kijiji cha Murray leo tarehe 10 Disemba 2024.
Mhe. Tango amesema kufuatia uwepo wa matukio ya ukatili wa Kijinsia katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu bado Serikali inajukumu kubwa la kuendelea kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa makundi yote kupitia mikutano ya hadhara, katika shule za Msingi na Sekondari, kufanya makongamano na mijadala, kushirikisha Taasisi mbalimbali zikiwemo za Dini pamoja na kuimarisha kamati ya Mtakuwa zilizopo katika ngazi Halmashauri, Vijiji na mitaa ili kuwa na uelewa kwa wote kuhusu ukatili
“Uwepo wa matukio ya ukatili inaonesha jinsi ambavyo tunapaswa kuendelea kujipanga na kutoa elimu kuhusu ukatili, na kuwepo na usaidizi wa utoaji elimu kwa rika zote katika maeneo yote ambayo matukio haya yamekuwa yakiripotiwa na hatimaye tuweze kufanikiwa kutokomeza ukatili”
Maadhimisho ya siku 16 za Kupinga Ukatili Yamekuwa na Kaulimbiu isemayo”Kuelekea miaka +30 ya BEIJING Chagua kutokomeza ukatili wa Kijinsia”
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.