Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amesema Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma zote muhimu karibu na maeneo yao.
Mhe. Prof. Mkumbo amesema hayo leo akiwa kwenye Ziara ya uzinduzi wa miradi ya Maendeleo Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara.
“Serikali imefikisha huduma ya Umeme kila kijiji nchi nzima na sasa imeanza kusambaza kwenye Vitongoji, lengo ni kuhakikisha inafikisha huduma zote muhimu kwa wananchi iwe ni upande wa Afya, Elimu, miundombinu, nishati na maeneo mengine”. Amesema Mhe. Kitila
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini Mhe. Zakaria Isaay ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayosimamiwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi mingi ya maendeleo Jimboni kwake na kusaidia wananchi kuondokana na changamoto mbalimbali
“Miradi iliyoletwa hapa Jimbo la Mbulu Mjini imesaidia wananchi wetu kujikwamua kiuchumi kwa sababu ya upatikanaji wa huduma muhimu kama Umeme, Maji, Elimu na Afya ambapo kwa kiasi kikubwa wananchi hawa wameona jitihada za Serikali zinavyofanyika”. Mhe. Issay
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo amefanya ufunguzi wa mradi wa mabweni mawili, madarasa 6 na matundu 9 ya vyoo katika shule ya Sekondari Kainam
Pia amezindua mradi wa kusambaza Umeme katika shule ya Sekondari Silaloda na Zahanati ya Silaloda ambayo imekuwa mkombozi mkubwa katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi wa Silaloda.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.