Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendiga leo Julai4,2025 amefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo itakayotembelewa,kukaguliwa na kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2025 katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Akiwa katika Ziara hiyo Mhe.Sendiga amewasisitiza viongozi wote kushirikiana ili kuhakikisha maandalizi yote yanakamilika kwa wakati ili kuupokea Mwenge wa uhuru.
Aidha Mhe.Sendiga ameongeza kuwasisitiza Wananchi wa Wilaya ya Mbulu kujitokeza kwa wingi kupokea Mwenge wa Uhuru.
Mwenge wa Uhuru 2025 unatukumbusha kulinda amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025 na kauli mbiu isemayo "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu"
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe.Michael Semindu ametoa shukurani za dhati kwa Mkuu wa Mkoa kwa kukagua na kuridhia miradi ya maendeleo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025.
Halmashauri ya Mji wa Mbulu inatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru julai16,2025 kutoka katika Halmashauri ya Mji wa Wa Babati.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.