Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewakumbuka watoto wenye mahitaji maalumu wanaosoma shule ya Msingi Endagkot kwa kuwapati mahitaji muhimu msimu huu wa sikuu ya mwaka mpya.
Mhe. Samia ametoa zawadi yake ya upendo kwa watoto hao ambao watafurahi sikuu ya mwaka mpya kwa kula vyakula kutoka kwake kama zawadi ambayo ameitoa kupitia Ofisi ya Mkoa wa Manyara iliyowakilishwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mbulu kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Mhe. Veronica Kessy.
Akikabidhi zawadi hizo Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Bw. Paulo Bura amewamshukuru Mhe. Rais kwa upendo wake kwa wanafunzi hao ambapo amesema zawadi hizo zitawafanya kuhisi upendo mkubwa ndani yao kutoka kwa Rais wao mpendwa.
Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi. Rehema Bwasi ametoa shukurani zake za dhati kwa Mheshimiwa Rais kwa upendo wake kwa watoto hao ambao mahitaji hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa kufurahi msimu huu wa kuelekea sikuu ya mwaka mpya na hata baada ya sikukuu hiyo kuisha.
Kwa niaba ya wazazi wa watoto wanaosoma shule ya Msingi Endagkot Bw. Pius Daniel amemshukuru Mhe. Rais kwa mchango wake kwa watoto hao na kuiomba Serikali iwasaidie kuwaongezea walimu wa kuwafundisha watoto hao wenye uhitaji maalumu.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.