Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi.Rehema Bwasi amekabidhi kadi za Pikipiki Kwa Kikundi Cha Vijana kinachojulikana kama Boda Tuzo ambacho ni miongoni mwa wanufaika wa Mikopo ya 10% Kwa mwaka wa Fedha 2022/2023
Akizungumza na Vijana hao Bi.Rehema amewapongeza vijana Kwa uzalendo na kujiamini Kwa kuhakikisha fedha zinarejeshwa Kwa wakati na Kwa usahihi mkubwa.
"Nyie ni Vijana wa Mfano nendeni mkawe vijana wa Kuigwa tumieni Pikipiki zenu kujiongezea kipato na mkawaelmishe vijana wengine faida za mkopo unaotolewa na Serikali".Alisema Bi.Rehema.
Aidha,ametoa shukrani Kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha Kwaajili ya Mikopo ya Wanawake,vijana na Watu wenye ulemavu.
Miongoni mwa Vijana wa Kikundi Cha Boda Tuzo Ndugu.Renald Gwandu ameishukuru Serikali kwa Kutoa Fedha zisizokuwa na Riba,ameeleza kuwa mikopo imesaidia vijana wengi kutokujihusisha na matendo yasiyofaa.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.