Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi. Rehema Bwasi amezindua mashindano ya umoja wa michezo na Taaluma kwa Shule za msingi Tanzania (UMITASHUMTA) kwa ngazi ya Halmashauri.
Akizungumza katika uzinduzi wa UMITASHUMTA amewaasa Washiriki kuonyesha vipaji vyao ili waende kuipeperusha vyema bendera ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
“Niwaase tushiriki mashindano kwa moyo kwani ni namna ya kukuza vipaji vyetu wenyewe kila mmoja ahakikishe ana kuwa na lengo la ushindi”. Alisema Bi. rehema.
Aidha, amewasisitiza washiriki wote kuendelea kutii mafunzo yote kadri ambavyo wataalamu watakuwa wakiwafundisha.
Mashindano ya UMITASHUMTA kwa Halmashauri ya Mji wa Mbulu yanahusisha shule zote za Msingi ambapo kwa ngazi ya Halmashauri yatafanyika kuanzia tarehe 26/05 hadi 27/05/2025 kwa ngazi ya Wilaya yanatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 28/05 hadi 29/05/2025 na kuhitimishwa tarehe 30/05/2025 kwa ngazi ya Mkoa wa Manyara.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.