Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi. Rehema Bwasi alipowatembelea Wanawake waliojifungua katika Hospitali ya Mji wa Mbulu.
Bi. Rehema amekutana na wanawake hao leo tarehe 6 Aprili, 2025 na kuwapa mkono wa pole na pongezi kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo mavazi.
Wakati huohuo ameagiza Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kuwatembelea wakina mama mara kwa mara ili kujua changamoto zinazowakabili na mahitaji yao ili waweze kusaidiwa kama sera ya Ustawi wa jamii inavyohitaji.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.