Kuelekea Maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Wananchi Wilayani Mbulu Mkoani Manyara wametakiwa kuenzi juhudi zilizofanywa na Waasisi wa Muungano huo
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Ndugu Paulo Bura akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbulu leo Aprili 25,2025 katika Zoezi la upandaji wa miti katika Shule ya Sekondari Isale ikiwa ni ishara ya kuenzi mambo yaliyofanywa na waasisi wa Muungano.
“Sherehe hizi za maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano zinatupa taswira ya tulikotoka, tulipo na tuendako hivyo basi ni jukumu letu ni kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya Muungano wa Tanzania.”Alisema Ndugu. Bura
Sambamba na hayo Ndugu. Bura ameeleza kuwa lengo la serikali ni kusogeza huduma karibu na wananchi na amewasisitiza Wananchi kuendelea kutunza miundombinu ambayo serikali imetoa fedha nyingi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mhe. Peter Sulle ameishukuru Serikali kwa kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi,amesema kumekuwa na maendeleo makubwa mpaka kufikia miaka 61 ya Muungano.
Jumla ya miti mia tano (500) ya mbao, matunda, urembo na kivuli imepandwa na Watumishi wa Wilaya ya Mbulu, Wanafunzi, yombo vya Usalama vya Wilaya na Wananchi katika Shule ya Sekondari Isale.
Zoezi la upandaji miti limetanguliwa na maandamano ya Awamu yaliyoongozwa na Vyombo vya usalama vya Wilaya ya Mbulu ikiwemo magereza,Polisi na uhamiaji.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.