Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu leo Juni 26,2025 ameongoza kikao cha Maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya kilichojuisha Halmashauri Mbili za Wilaya ya Mbulu yaani Halmashauri ya mji na Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Semindu amewasisitiza wakuu wa idara,Vitengo na Wakuu wa Taasisi kuendelea kushirikiana katika maandalizi ya Mbio za Mwenge wa uhuru 2025.

“Ili tuweze kufanikiwa katika Mapokezi ya mwenge wa Uhuru 2025 nguzo kubwa ni ushirikiano tusikubali kuachana ”Alisema Mhe. Semindu
Sambamba na Hayo Mhe. Semindu amesisitiza kuendelea kuwahamasisha Wananchi kujitokeza na Kushiriki katika Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Wilaya ya Mbulu inategemea kupokea Mwenge wa Uhuru tarehe 16/07/2025 kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati na Kukimbizwa katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu 17/06/2025 Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.