.
Wataalamu wa Bima ya Afya leo, tarehe 16 Februari 2026, wametoa elimu kuhusu Bima ya Afya kwa Wote kwa wananchi wa Kata ya Ayamaami, Mtaa wa Hayahaya, ikiwa ni sehemu ya juhudi endelevu za kuhamasisha jamii kuelewa umuhimu wa kuwa na kinga ya kifedha dhidi ya changamoto za kiafya.
Katika utoaji wa elimu hiyo, wananchi walielimishwa kuhusu faida mbalimbali za kujiunga na bima ya afya, zikiwemo upatikanaji wa huduma za matibabu kwa gharama nafuu, kuepuka mzigo wa gharama za ghafla pindi ugonjwa unapotokea, pamoja na kuhakikisha familia zinapata huduma bora za afya kwa wakati unaofaa.
Aidha, wataalamu hao waliwahimiza wananchi kutumia fursa ya mpango wa Bima ya Afya kwa Wote kwa kujiandikisha mapema, kama hatua muhimu ya kujilinda dhidi ya hatari za kiafya na kuchangia kwa vitendo kuboresha ustawi wa jamii kwa ujumla.
HABARI KATIKA PICHA.



Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.