Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mhe. Peter Sulle ameupongeza uongozi wa Halmashauri pamoja na walimu kwa usimamizi mzuri upande wa Elimu na kupelekea ufaulu wa kidato cha nne kufikia 99.62%.
Pongezi hizo zimetolewa leo mbele ya Mkutano wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2025/2026 ambapo amesema walimu wameonyesha uzalendo na jitihada kubwa katika kuhakikisha wanafunzi Kidato cha nne kwa mwaka 2024 wanafaulu vizuri katika masomo yao.

Pamoja na hayo Mhe. Sulle amesema wakati Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan inajenga miundombinu bora na kuwezesha mazingira rafiki ya wanafunzi kujisomea, shauku ya Rais ni kuona fedha zinatumika ipasavyo kwa kuweka mazingira rafiki ya kujisomea.
Watahiniwa takribani 1,577 walifanya mtihanj wa kuhitimu Kidato cha nne 2024 na kupata ufaulu wa 99%.

Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.