Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu amewataka wateule wa Rais, Madiwani na watumishi wa Umma kuhakikisha wanatoa mrejesho wa shughuli za wananchi zinazohusu shughuli za maendeleo kwa wakati.
Mhe. Semindu amesema hayo mapema leo Februali 21, 2025 akiwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la kawaida lililofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri.
Mhe. Semindu amesema kila mtu anapaswa kuwajibika kwa Wananchi kwa kuhakikisha anatoa mrejesho wa kazi zinazofanywa kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na kusoma mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu kuanzia ngazi za Vijiji.
“Sisi wateule wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Viongozi mliochaguliwa kwa kupigiwa kura (Waheshimiwa Madiwani), Watumishi wa Umma mpaka ngazi za Vijiji niwaambie sisi mabosi wetu ni wananchi kwa hiyo lazima tuwajibike kwa kuwatumikia ipasavyo”
“Ni jukumu letu kama viongozi kumsaidia Mhe. Rais katika kuwatumikia wananchi wetu ambao wanatarajia kupata maendeleo katika sehemu zote muhimu katika upande wa Afya, Elimu, Umeme, Miundombinu na maeneo mengine kwa sababu hawezi kufika kila kijiji…hivyo sisi tuliopo ngazi za chini lazima tuseme yanayofanyika” Alisisitiza Mhe. Semindu
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.