Timu ya Uratibu wa Mbio za Mwenge wa uhuru 2025 kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara imeipongeza Halmashauri ya mji wa Mbulu kwa Maandalizi ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
Akizungumza Katibu Tawala Msaidizi ( Mhandisi) Bi. Lydia Massoro ameeleza kuwa kazi ya usimamizi wa Miradi ya maendeleo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2025 inaonekana ikifanyika.
“ Niwapongeze sana kwa maandalizi ya mapokezi ya mbio za mwenge wa uhuru 2025, tuendelee kuboresha zaidi na kurekebisha dosari ambazo zimejitokeza katika miradi yetu inayotekelezwa”. Alisema Bi. Lydia
Kwa upande wake katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Ndugu. Paulo Bura ameahidi kuendelea na maandalizi kwaajili ya mapokezi ya mwenge wa uhuru ikiwemo ufuatiliaji wa nyaraka mbalimbali za miradi ya maendeleo.
Nae Mkurugenzi Wa Halmashauri ya mji wa mbulu Bi. Rehema Bwasi
ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kipindi ambacho maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru yanaendelea.
Halmashauri ya Mji wa Mbulu inatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru tarehe 16/07/2025.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.