Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwa kuendelea kupata Hati safi.
Akizungumza leo tarehe 28 Mei, 2025 katika Mkutano Maalumu wa Baraza la Kujibu hoja za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mhe. Sendiga ameeleza kuwa matokeo ya kupata hati safi ni pamoja na ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo.
“Wataalamu endeleeni kusimamia majukumu ipasavyo hususani suala zima la usimamizi wa Miradi ya Maendeleo pamoja na Ukusanyaji wa mapato ya Serikali”.Alisema Mhe. Sendiga
Sambamba na hayo Mhe. Sendiga ameongeza kwa kuwasisitiza Wataalamu kuendelea kuzingatia miongozi ya Serikali ikiwemo matumizi ya mifumo ya Manunuzi.
Halmashauri ya Mji wa Mbulu ilikuwa na hoja thelathini na Sita (36) zilizofutwa ni hoja Kumi na sita (16) na hoja ishirini (20) Ziko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.



Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.