Uzinduzi wa mashindano ya Umitashumta na Umisseta Mkoa Iringa 2025.yenye kauli mbiu isemayo
" Viongozi Bora ni msingi wa Maendeleo ya Taaluma sanaa na michezo, Shiriki uchaguzi Mkuu 2025 kwa Amani na utulivu.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amefungua Rasmi mashindano ya Umitashumta na Ummisseta yanayojumuisha Mikoa yote 26 Nchini ,Katika uzinduzi huo ameipongeza Ofisi ya Rais Tamisemi na Wizara ya Habari kuendelea kuhakikisha michezo inafanyika kila mwaka ,pia ameupongeza Uongozi wa Mkoa wa Iringa kwa maandalizi mazuri ya viwanja na malazi.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa kauli mbiu imebeba ujumbe mzuri unaohamasisha michezo na shughuli za maendeleo na amewataka wanamichezo kuonesha umahiri katika michezo ili michezo iwe na tija kwenye maisha yao katika kujenga Afya, kuepuka ulevi, madawa ya kulevya,utoro shuleni, kupata ajira na kuongeza mapato.
Aidha ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha mikakati ya michezo ambapo takribani bilioni 11 zimetengwa kuimarisha miundombinu ya michezo katika Shule 10 Nchini, billioni 32 zimetengwa kuimarisha Chuo Cha Malya ambacho kitakuwa kikubwa Afrika Mashariki kwa ajili ya kuandaa wanamichezo, mfuko wa Maendeleo ya michezo kwa ajili ya kuendeleza vipaji,pia
Serikali imejipanga kufundisha kwa nadharia na kwa vitendo michezo.
"Vyama vya michezo mlete wataalamu katika mashindano haya ili waweze kuibua wanamichezo, ameeleza.
Pia amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote kuhakikisha Walimu wa michezo wanapata mafunzo yanapotokea, pia maeneo yaliyowazi kutumika kwa ajili ya matumizi ya michezo
Wizara ya Utamaduni kutoa vibali kwa Shule binafsi vya uendelezaji wa vipaji , watanzania wote kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha Afya.
Sambamba na hilo amewataka wananchi kushiriki uchaguzi kwa Amani na utulivu kwa kuwa uchaguzi utakuwa wa huru na wa haki
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Peter Serukamba amewakaribisha wanamichezo wote na ameeleza kuwa hali ya ulinzi na usalama Mkoa wa Iringa ni shwari.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.