MAKARANI WAONGOZAJI 274 WAPATIWA MAFUNZO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU JIMBO LA MBULU MJINI
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbulu Mjini, Ndugu Philemon Maffa, ameendesha mafunzo kwa jumla ya makarani waongozaji 274 wa vituo vya kupigia kura leo Oktoba 25, 2025, ikiwa ni hatua muhimu ya maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Ndugu Maffa aliwataka makarani hao kufanya kazi kwa uzalendo ili kuhakikisha zoezi la uchaguzi.
“Niwakumbushe kuviishi viapo vyetu katika utekelezaji wa majukumu yetu, kwani Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetuamini kusimamia mchakato huu muhimu,” alisema Maffa.
Aidha, Ndugu. Maffa amewahimiza kuwa waadilifu na kutekeleza majukumi yao kwa weledi ili kihakikisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unafanyika kwa haki, amani na utulivu.
Katika hatua nyingine, makarani wote 274 wamekula kiapo cha kutunza siri na kujivua uanachama wa vyama vya siasa, kama sehemu ya maandalizi ya rasmi ya utekelezaji wa majukumu yaokatika Uchaguzi Mkuu.

Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.