Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya mji wa Mbulu wamepatiwa Mafunzo ya namna ya utumiaji wa Mfumo wa Manunuzi (Nest).
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Ndugu Gidion Kitoboli amewataka Wataalamu wote kuwa makini katika mafunzo hayo na kutoa ushirikiano ili kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiibuka katika mfumo wa manunuzi mara kwa mara.
“Tumekutana na changamoto mara kwa mara kwenye mfumo wa manunuzi kwa kila mmoja ni muda sahihi wa kupata utatuzi wa changamoto hizo kutoka kwa Wataalamu wetu kutoka Mamlaka ya Uthibiti Ununuzi wa Umma ( PPRA) ”. Alisema Ndugu. Kitoboli.

Kwa upande wake Afisa Kutoka Mamlaka ya Uthibiti ununuzi wa Umma (PPRA) Bi. Nuru Bazaar amewakumbusha Wataalamu kuzingatia utaratibu wa Serikali wa ununuzi ili kurahisisha utendaji wa Taasisi katika suala zima la Manunuzi.
Mafunzo ya Mfumo wa Manunuzi ( NEST) yametolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo Watalamu katika Taasisi juu ya taratibu za ununuzi wa Umma kwa kufuata taratibu za Mfumo wa Manunuzi( NEST).


Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.