Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Mbulu wamepatiwa mafunzo ya namna ya uendeshaji wa Kampuni Tanzu yenye lengo la kuongeza mapato ya Halmashauri.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uendeshaji wa kampuni tanzu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mhe. Peter Sulle amesema ni vyema kila mmoja kushiriki mafunzo hayo ili kuweza kutoa ushauri na kufanya maamuzi ya pamoja kwa ajili ya kujenga Halmashauri.
“Haikuwa vyema kwamba mafunzo haya yakapatiwa kwa watu wachache ndiyo maana imebidi watu wote tufike tujifunze kw a pamoja ili tuwe huru kuwa kufanya maamuzi kwa pamoja”.Alisema Mhe.Sulle
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Ndugu Ally Msangi amewapongeza Waheshimiwa Madiwani kwa kujitokeza na amesema mafunzo haya yatatupa Ushirikiano na kuweza kufanya maamuzi yaliyosahihi kwa Maendeleo ya Halmashauri.
Mafunzo ya Namna ya uendeshaji wa Kampuni tanzu yametolewa kwa Waheshimiwa Madiwani wote wa Halmashauri ya mji wa Mbulu.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.