Wauguzi wa Halmashauri ya mji wa Mbulu wameungana na wauguzi wote nchini kuadhimisha siku ya wauguzi duniani leo tarehe 12/05/2025.
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na utoaji wa zawadi kwa kwa wagonjwa waliopo katika Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Mbulu.
Wauguzi wameaswa kuyaishi maadili ya uuguzi kama ilivyo katika viapo vyao kwa kwakuwahudumia wagonjwa kwa mioyo ya upendo na huruma.
Zoezi hilo liliongozwa na Muuguzi Mkuu wa Halmashauri mji wa mbulu Bi. Subira Mathiya.
Maadhimisho ya siku ya Wauguzi duniani yamekuwa na kauli mbiu isemayo “Uuguzi nguvu ya Mabadiliko;Huduma bora Wajibu wangu”
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.