Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbulu ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe.Michael Semindu imefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru Mwaka 2025.
Akizungumza katika ziara hiyo Mhe.Semindu amewasisitiza Wataalamu kuendelea kufanya maandalizi kwaajili ya kupokea Mwenge wa uhuru.
"Kila mmoja kwa nafasi yake aendelee kuwajibika ipasavyo katika maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2025, ushirikiano ndicho kitu pekee kitatufanya kukamilishe maandalizi yetu".alisema Mhe.Semindu
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Bi.Rehema Bwasi ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano ili kufanikisha maandalizi ya Mbio za Mwenge wa uhuru.
Miradi iliyotembelewa ni mradi wa Daraja la kamba kijiji cha Tsawa,Mradi wa maji kata ya Uhuru,Mradi wa Shule mpya ya Sekondari ya Amali Gunyoda,Hoteli ya mwananchi,Mradi wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia chuo cha maendeleo ya Wananchi Tango,Ujenzi wa uzio wa Bweni la Wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalumu katika shule ya Msingi Endagkot,Jengo la Mama na mtoto katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Kikundi cha vijana(Sankara group) 10%.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.