Kamati ya Siasa ya Wilaya Mbulu imepongeza utekelezaji wa miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbulu Comredi Melkiadi Naari, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu, Wakuu wa Taasisi na Wataalamu wakiongozwa na Wakurugenzi wa Halmashauri wametembelea na kukagua maendeleo ya miradi katika sekta ya Elimu, Afya n.k na kujionea jinsi ambavyo Serikali imewekeza fedha nyingi kwa nia ya kusogeza huduma karibu na wananchi.
Kamati hiyo ikiwa katika ukaguzi huo imesisitiza miradi inayoendelea kutekelezwa kukamilika kwa wakati ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.
Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu amewasisitiza Wataalamu kuendelea kujituma ili kuunga juhudi za Serikali kwa fedha zinazoletwa kwaajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo.
Miradi iliyotembelewa katika Halmashaurinya Mji wa Mbulu ni Shule mpya ya Sekondari Issale,Shule ya Sekondari Ayamohe , Mradi wa Daraja la Kamba za Chuma lililopo Kitongoji cha Tipri kata ya Gehandu na Ujenzi wa Daraja lililopo Kata ya Silaloda.
Miradi iliyotembelewa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ni pamoja Mradi wa maji Masqaloda,Shule ya Amali iliyoko kijiji cha Harsha kata ya Bashay na Ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa Nje,Upasuaji na jengo la utawala la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.