Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Manyara Leo tarehe 12 Mei,2025 ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa manyara Ndg. Peter Toima imefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani katika Wilaya ya Mbulu.

Kamati hiyo imekagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mbulu Mji yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1. Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa madaraja na matengenezo barabara ya Silaloda – Harbanghet Km 11.5 na Ukarabati wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu.
Kupitia ziara hiyo Ndugu.Toima amempongeza Mkuu wa Mkoa Mhe.Queen Cuthbert Sendiga na ameeleza Chama kimeridhishwa na Miradi ya maendeleo ilivyotekelezwa katika Halmashauri hizo.


Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.