Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu imekagua miradi mbalimbali ya Maendeleo na kuagiza ikamilike kwa wakati ili iweze kuwanufaisha Wanachi.
Kamati hiyo imefanya ziara hiyo leo Aprili 23,2025 ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Alex Tango akiwa na wajumbe ambao Waheshimiwa madiwani na Wataalamu wa Idara na vitengo mbalimbali.
Kamati hiyo imeagiza kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati, wakandarasi kuwa waaminifu ili thamani ya Fedha iendane na uhalisia wa miradi husika.
Sambamba na hayo kamati ya Fedha na Utawala imeagiza Watoa huduma katika Zahanati ya Bargish Uwa kuendelea kutoa huduma kwa uaminifu ili kuunga mkono juhudi za Serikali kwani serikali imetoa fedha nyingi kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu ya afya.
Miradi iliyotembelewa ni Ujenzi wa mabweni mawili (02) shule ya Sekondari Marrangw,Ujenzi wa Shule mpya ya Amali Gunyoda, ujenzi wa Karakana katika shule ya Msingi Endagkot.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.