HATI MILIKI 48 ZA ARDHI ZATOLEWA KWA WANANCHI WA HALMASHAURI YA MJI WA MBULU.
Oktoba 9,2025, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu ameshiriki katika Kliniki maalumu ya kushughulikia changamoto,kero na kukabidhi hati miliki za ardhi kwa Wananchi wa Halmasshauri ya Mji wa Mbulu.
Akizungumza na Wananchi wa Mbulu Mhe. Semindu amewasitiza wananchi juu ya muhimu wa hati miliki kwani ameeleza kuwa huonyesha uhalali katika umiliki wa ardhi.
“Katika jamii yetu kumekuwa na migogoro mingi ya ardhi, ili kuepusha migogoro ni muhimu kila mwananchi akawa na hati miliki”.alisema Mhe. Semindu
Aidha, Mhe.Semindu aliwasisitiza wananchi Kutokujichukulia sheria mkononi pale amabapo changamoto za ardhi zinajitokeza katika maeneo wanaishi. Aliwasisitiza wananchi kuwaona wataalamu ili kupata msaada wa kitaalamu.
Kwa niaba ya Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Manyara Ndugu.Masawika Kachenje amewasisitiza wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu kuendelea kuwatumia wataalamu wa ardhi ili kutatua changamoto zinazojitokeza katika jamii.
Kliniki maalumu imehusisha usikilizaji na utatuaji wa changamoto za wananchi katika masuala ya ardhi.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.