DC SEMINDU AWASISITIZA WATENDAJI KUENDELEA KUSHIRIKIANA KATIKA UTEKELEZAJI WA AFUA ZA LISHE.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Michael Semindu, amewataka watendaji wa kata na wataalamu wa lishe kuendelea kushirikiana kwa karibu katika utekelezaji wa afua za lishe ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za lishe na wilaya inaendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa mikakati hiyo.
Wito huo umetolewa Oktoba 21, 2025, katika kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/2026.
“Tunatakiwa kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa afua za lishe ili tuhakikishe tunafikia malengo yaliyowekwa katika afua za lishe,” alisema Mhe. Semindu.
Aidha, alitumia fursa hiyo kuwasisitiza watendaji kuwahamasisha wananchi kujitokeza kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu, Ndugu Paulo Bura, alisema suala la lishe ni ajenda ya kitaifa, hivyo kila mtendaji anapaswa kulitilia mkazo katika utekelezaji wa shughuli za shule.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu, Ndugu Rehema Bwasi, aliahidi kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wataalamu wa lishe kutekeleza majukumu yao, huku akiwataka kuwasilisha taarifa za changamoto wanazokutana nazo ili zipatiwe ufumbuzi kwa wakati.
Copyright ©2020 GWF . All rights reserved.